SHINIKIZO LA JUU LA DAMU (HYPERTENSION)
Ugonjwa wa shinikizo la juu la damu
ambao kwa lugha ya Kitaalamu huitwa “Hypertension” au kwa lugha ya Kigeni “High
Blood Pressure”. Ugonjwa huu ni moja
ya magonjwa yanayowaathiri watu duniani kutokana na mateso,vifo pamoja na
gharama zinazoambatana nao.Ugonjwa huu umekuwa ni moja ya changamoto muhimu
katika afya ya jamii
Kwa kawaida wakati moyo ukisukuma damu katika ateri (mishipa midogo ya damu),damu hiyo hupita kwa nguvu dhidi ya kuta za mishipa hiyo.

Shinikizo la damu la kawaida kwa watu wengi ni milimita za mekyuri 120/80 .Chini ya hapo huitwa shinikizo la chini
la damu (hypotension) na juu ya kipimo hicho huitwa shinikizo la juu la
damu (hypertension) ambalo huanzia milimita za mekyuri 140 kwa “systolic
pressure” milimita za mekyuri 90 kwa “diastolic pressure”.
Nini husababisha shinikizo la damu?
Kuna aina mbili za shinikizo la juu la damu ;
a)Shinikizo la juu la damu la lazima (Essential Hypertension)
Aina hii ya shinikizo la juu la damu huathiri kati ya asilimia 90-95% ya watu wanaougua shinikizo la juu la damu.Kuna baadhi ya vigezo vinaorodheshwa kuhusika na shinikizo hilo la juu la damu.
Vigezo visivyoepukika:
i)Umri:Kadri umri unavyoongezeka ndivyo uwezekano wa kupata shinikizo la juu la damu unavyozidi kuwa mkubwa kwa sababu kuta za mishipa ya damu huzidi kuwa ngumu hivyo kushindwa kutanuka kirahisi na kuongeza shinikizo (pressure)
ii)Asili (Race): Jamii ya watu weusi (waafrika) wana hatari kubwa zaidi kupata shinikizo la damu kuliko watu weupe.
iii)Histori a ya Kifamilia (Kurithi): Imegundulika kuwa uwezekano wa ndugu kupata shinikizo la juu la damu ni mkubwa iwapo ndugu wengine katika familia wamekwishawahi/wanaugua ugonjwa huo.
iv)Jinsia:Wanaume wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata shinikizo la juu la damu kuliko wanawake.

Vigezo vinavyoepukika:
Hivi ni vile ambavyo kwa lugha nyingine vyaweza kuepukwa;-
i)Unene wa kupita kiasi: Unene wa kupita kiasi ni uzito wa zaidi ya “body mass index” (BMI) 30kg/m2 (BMI =uzito (kwenye kg) ÷ Urefu (kwenye mita)2 )
ii)Kiwango cha chumvi (sodium) mwilini : Baadhi ya miili ya watu hugundua haraka kiwango cha chumvi (sodium) na shinikizo lao la damu hupanda punde watumiapo chumvi.Kupunguza matumizi ya chumvi husaidia kupunguza shinikizo la damu. Vyakula vya -viwandani na madawa ya kupunguza maumivu huwa na kiasi kikubwa cha madini ya chumvi “sodium”
iii)Vidonge vya majira: Baadhi ya wanawake wanaotumia vidonge vya uzazi wa majira hupata shinikizo la juu la damu.
iv)Kutokufanya mazoezi: Kutokufanya mazoezi ni moja ya sababu zinazopelekea unene wa kupita kiasi (obesity).
v)Madawa: Baadhi ya madawa kama Amphetamines huweza kupandisha shinikizo la damu.
b)Shinikizo la juu la damu litokanalo na magonjwa mengine (Secondary hypertension)
Aina hii ya shinikizo huathiri karibu asilimia 10 ya watu.Hutokana na magonjwa mengine kama:
i)Magonjwa sugu ya figo
ii)Uvimbe kwenye tezi za figo (adrenal gland)
iii)upungua kwa upana wa mshipa mkuu utoao damu kwenye moyo kwenda mwilini (coarctation of aorta)
iv)Ujauzito
v)Matumizi ya vidonge vya majira
vi)Matumizi ya kupita kiasi ya pombe
vii)Kutokufanya kazi kwa tezi mdundumio (thyroid gland dysfunction)
viii)Madawa na sumu (kokeini)

Dalili za Shinikizo la Juu la Damu
Kwa kawaida Shinikizo la juu la damu huwa halionyeshi dalili na kama zikitokea basi huwa kwa kiasi kidogo na zisizo maalum na ndio maana ugonjwa huu huitwa “Muuaji wa Kimya kimya” (Silent Killer).Watu wenye Shinikizo la juu la damu huwa hawajifahamu mpaka wanapopimwa.

Baadhi
ya watu wenye shinikizo la juu la damu huwa na dalili zifuatazo:
a)Maumivu ya Kichwa
b)Kizunguzungu
c)Kutoona sawasawa
d)Kichefuchefu
e)Kichomi
f)Kuchoka haraka
Uchunguzi na Vipimo
Kupima Shinikizo la damu kwa kutumia Mashine ya Kupimia Presha ili kujua kama ni zaidi ya Milimita za Mekyuri 140/90.
Damu: Kuangalia kiwango cha Yurea (urea),madini (electrolytes) na Krietinini (Creatinine

Moyo: Kutanuka kwa ventriko ya kushoto ya moyo (left
ventricular hypetrophy) ambayo kupungua kwa kiwango cha damu kisukumwacho na
moyo, maumivu ya moyo (Angina Pectoris).
Mishipa ya damu:
kuharibika kwa mishipa (diffuse atherosclerosis
Kinga
i)Jali uzito wako kwa kutonenepa kupita kiasi
ii)Kufanya mazoezi pia hupunguza uzito
iii)Punguza kiwango cha chumvi kwenye chakula
iv)Acha kunywa pombe
vi)Kula mlo wenye matunda na mboga za majani zaidi.,
vi)Punguza vyakula vyenye mafuta haswa lehemu (cholesterol)
vii)Acha kuvuta tumbaku (sigara)
viii)Punguza msongo wa mawazo (stress) kwa kufanya mazoezi.

Matibabu na Ushauri
-Shinikizo la juu la damu ni ugonjwa wa muda mrefu (kudumu) na ili udhibitiwe, mabadiliko katika mwenendo wa kuishi (litestyle) na matumizi sahihi na endelevu ya dawa lazima yazingatiwe.Ni muhimu kujenga utamaduni wa kupima shinikizo la damu mara kwa mara kwa sababu mara nyingine dalili huchelewa kuanza kuonekana.

Dondoo za kubadili tabia
1. Tumia ngazi badala ya lifti
2. Paki gari mbali kidogo kutoka kwenye ofisi
3. Endesha baiskeli
4. Jishughlishe na bustani
5. Fanya usafi wa nyumba

Analysed by Dr Charles Sizya,
written by Paradise clinic
No comments:
Post a Comment