Chumvi- ni kiharibu madini: kama sukari ni sumu tamu, chumvi inazingatiwa
ama kiharibu madini. Matumizi ya chumvi kupindukia yanasababisha figo kuwa
dhaifu na hatimae kushindwa kufanya kazi zake.
Ni ukweli usiopingika kuwa chumvi ni
muhimu kwa ajili ya radha, lakini matumizi yake ya kupindukia yanaleta madhara
mwilini. Watu wengi wanaamini kuwa hawawezi kupika pasipokuwa na chumvi, ndio
maana ni vigumu kula pasipo chumvi. Kwa mujibu wa walaji, chumvi sio muhimu kwa
maisha na afya pia. Kwa maneno mengine
naweza sema hakuna maendeleo ya mwilini yanayotegemea chumvi.
Mwili wa mwanadamui unahitaji mbegu
mbili za chumvi(50grams) kwa sikuambayo tunaipata kupitia mboga. Mlo tunaopata
kutokana na matunda na mboga unatupatia chumvi ya asili na hauna hitaji la
kuongeza chumvi ya ziada.
Chumvi inamadhara makubwa kiliko faida,
mfanyakazi anaweza akahitaji chumvi kufidia ile iliyopotea kwa pumzi. Kama
asipoweka chumvi anaweza kupata maumivu
ya mwili, misuli kubana na uchovu.
Kuondoa kabisa matumizi ya chumvi katika
mlo itakuwa tiba ya kusinzia na kukoroma. Mtu anahangaika na shinikizo la juu
la damu atasaidika kama atapunguza matumizi ya chumvi katika mlo wetu, afya
zetu zitakuwa safi. Kwa upande mwingine, matumizi makubwa ya chumvi yatatupatia maradhi/magonjwa.
No comments:
Post a Comment