Monday, 20 June 2016

WALIOPATA NAFASI YA KAZI

Ninayo furaha kukutangazia kuwa baada ya kusubiri kwa muda mrefu, uchambuzi ulio fanywa na idara ya ajira paradise sanitarium clinic, inatoa matokeo kama ifuatavyo:-

maombi tuliyopokea
tumepokea maombi mbalimbali kutoka pande zote za africa mashariki(Tanzania, Kenya, na Uganda). jumla ya maombi tuliyopokea ni 347, ikiwa;- mwanza (23), tarime(70), musoma(15), bunda(8), dodoma(31), iringa(5), dar es salam(19), arusha(40), tabora(53), shinyanga(36), nairobi(17), simiyu(20), uganda(3), kagera,geita na bukoba(15).

waliochaguliwa
1.Happymachus Kimasha kutoka Tabora (herbs supply)
2.Joseph Sinda kutoka Serengeti (herbs supply)
3.Martha peter kutoka Tarime (herbs supply)
4.Evans Jacob Kutoka Arusha (clinical office)
5.Naomi Melizedeki kutoka Musoma(herbs supply)
6.Daniel Nyangira kutoka Tarime (herbs suplly)
7.Ladyanna Jacob kutoka Mwanza (reception)
8.Carolina Ojode kutoka Bunda (reception)
9.Thomas John kutoka Nairob (clinical office)



wote waliochaguliwa wafike ofisini tarehe mosi, July, aidha wale ambao hawajapata nafasi na wangependa kupata wafuatilie second selection mapema mwezi wa nane.


Sunday, 19 June 2016

KIFAFA CHA MIMBA




KIFAFA CHA MIMBA – PREECLAMPSIA, ECLAMPSIA.
Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaohusiana na msukumo mkubwa wa damu (high blood pressure) wakati wa ujauzito pamoja na kuharibika kwa viungo muhimu mwilini kama vile figo na ini. Kwa kawaida ugonjwa huu hutokea baada ya nusu ya kwanza ya ujauzito kuisha (kuanzia wiki ya 20 au miezi mitano ya ujauzito).
Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito.
Ugonjwa wa kifafa cha mimba unaweza kuleta madhara makubwa kwa mjamzito na mtoto aliye tumboni. Kuharibika kwa viungo muhimu kama figo na ini la mjamzito kunaweza kuwa kwa kiwango kikubwa kichoweza kusababisha mjamzito kupoteza maisha iwapo hatapata huduma ya afya mapema. Vilevile mtoto aliye tumboni anaweza kuathirika kwa kukosa damu ya kutosha toka kwa mama na kushindwa kukua vizuri na iwapo hali hiyo ikiendelea muda mrefu anaweza kufia tumboni.
Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto walio tumboni, inashauriwa kila mjamzito awe anahudhuria clinic na kupimwa msukumo wa damu (blood pressure) na mkojo ili kuhakikisha kuwa yuko salama.
Iwapo kipimo cha msukumo wa damu ni kikubwa kuliko 140/90 mmHg, ni muhimu kurudia kipimo hicho baada ya muda na kufanya vipimo vingine vya maabara vinavyoweza kujulisha uwepo wa kifafa cha mimba.
Kwa kawaida ugonjwa huu huwepo kwa muda fulani bila mjamzito kuona dalili zozote. Ghafla mjamzito anaweza kuanza kuona dalili kama maumivu ya tumbo juu ya kitovu, kutapika, macho kutokuona vizuri, kuumwa kichwa, mkojo kuwa na rangi tofauti na kawaida, kupumua kwa shida, uchovu na maumivu ya viungo au kupoteza fahamu na “degedege“.

Thursday, 16 June 2016

Friday, 10 June 2016

FAIDA ZA MWEMBE

ZIFAHAMU FAIDA ZA MWEMBE(embe)
Mti wa mwembe mbali ya kuzaa tunda la embe ambalo hutumika kama chakula au kinywaji ( juisi ) chenye ladha ninayo vutia, una faida lukuki za kiafya kwa mwili wa mwanadamu.
Zifuatazo ni baadhi ya faida za kiafya za mti wa mwembe.

1. MAJANI YA MTI WA MWEMBE :
Majani machanga ya mti wa mwembe yakichemshwa huwa na faida zifuatazo ;
i. Hutibu pumu
ii. Hutibu kifua kikavu
iii. Hutumika katika kuoshea vidonda vitokanavyo na majeraha mbalimbali ( Majani ya maembe yamethibitika kuwa na uwezo mkubwa wa kukausha majeraha ya vidonda )
iv. Unga wa majani ya mwembe hutumika katika kutunza meno ambapo mtu mwenye matatizo ya meno atatakiwa kusukutua kwa kutumia unga unaotokana na majani ya mwembe.

2. KOKWA LA EMBE
Unga unaotokana na kokwa la embe husaidia kuzuia kuharisha na kuhara damu.

3. T UNDA LA EMBE
i. Ulaji wa tunda la embe husaidia kutibu minyoo na kuzuia uvujaji wa damu ovyo.
ii. Tunda la embe lina vitamin C na hivyo ulaji wake husaidia kuponesha vidonda kwa haraka, hivyo basi mlaji sana wa tunda la embe endapo atapata vidonda basi atapona kwa haraka sana kuliko mtu asiye tumia tunda hili mara kwa mara.
iii. Huwasaidia watu wenye matatizo ya kutokupata choo.
iv. Utumiaji wa maembe mabichi husaidia kuondoa mawe kwenye figo na hivyo kuepuka kufanyiwa upasuaji.
v. Embe bichi likichanganywa na chumvi na sukari na kasha kuchemshwa ni tiba ya tatizo la mapigo ya moyo kwenda kwa haraka.

MAGOME YA MWEMBE
Magome ya mti wa mwembe yakichemshwa ni dawa nzuri ya homa.

JUISI YA EMBE :
Juisi ya embe ikichanganywa na maziwa ya soya husaidia kurejesha afya ya mtu aliye dhoofika.
Vile vile kunusa juisi ya embe kunasaidia kuzuia tatizo la kutoka damu puani. Hivyo basi juisi ya embe inaweza kutumika kama huduma ya kwanza kwa mtu anaye tokwa na damu puani

UGUMBA


Ugumba
           Ugumba ni hali inayotokea iwapo watu wawili, mwanaume na mwanamke wanapokutana kimwili (au kujamiana) bila kutumia njia yoyote ile ya upangaji uzazi kwa muda wa miezi 12 na kutoweza kushika mimba au kupata ujauzito.
KUNA AINA MBILI ZA UGUMBA;
Ugumba wa asili (Primary infertility) - Hii ni pale ambapo mwanaume na mwanamke hawajawahi kutunguisha mimba kabisa maishani mwao hata baada ya kujamiana au kukutana kimwili kwa muda wa mwaka mmoja bila kutumia njia yoyote ile ya kuzuia kupata mimba.
Ugumba unaotokea baadaye maishani (Secondary infertility) - Hii ni pale ambapo wote wawili, mwanamke na mwanaume wameshawahi kupata ujauzito au kutungisha mimba angalau mara moja maishani mwao na baada ya hapo hawajafanikiwa kupata au kutungisha mimba tena.
Asilimia 30-40 ya tatizo la ugumba huwakumba wanaume na asilimia 40-50 ya tatizo hili huwakumba wanawake, wakati asilimia 10-30 zilizobakia ya tatizo hili husababishwa kwa pamoja na matatizo kati ya wanaume na wanawake, hapa sababu halisi hazijulikani.
Kwa wale wenye afya njema, uwezekano wa kupata au kutungisha mimba iwapo watajamiana mara kwa mara kwa mwezi ni asilimia 25-30. Wanawake hufikia kilele cha kupata ujauzito (peak fertility) wakiwa kwenye miaka ya ishirini. Mwanamke aliye na umri wa zaidi ya miaka 35 (au baada ya miaka 40) ana uwezekano wa kupata ujauzito kwa asilimia 10.
   

UTUNGWAJI WA MIMBA
   Mimba hutungwa baada ya mwanamke kutoa yai kutoka katika moja ya viwanda vyake vya mayai ya kike yaani ovaries, kitendo hiki hujulikana kama ovulation. Yai husafiri hadi kwenye mfuko wa uzazi ujulikanao kama uterus (womb) kupitia kwenye mirija ya uzazi inayojulikana kama mirija ya fallopian.
Mbegu moja ya kiume (sperm) ni lazima itungishe au iungane (fertilize) na yai au mayai ya kike (ovum au ova) wakati yai likielekea kwenye uterus. Baada ya mbegu ya kiume na yai la kike kuungana, muunganiko uliotengenezwa yaani kiinitete (embryo) hushuka mpaka kwenye mfuko wa uzazi na kujiwekeza hapo ili kiendelee kuwa kiumbe.
Tatizo la ugumba linaweza likawa ni la nwanaume au mwanamke pekee ingawa wakati mwingine wote wawili wanaweza kuwa na tatizo hili.
Ni sababu zipi zinazoleta tatizo la ugumba (infertility) ?
Kwa wanawake ;
Tatizo la ugumba linaweza kutokea wakati wa;
Yai au kiumbe kilicho ndani ya mfuko (uterus) wa uzazi kushindwa kukua hadi kufikia kuwa mtoto.
Mayai yaliyo ndani ya mfuko wa uzazi kushindwa kujishikiza kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi (uterus lining)
Matatizo kwenye njia ya kupita yai au mayai wakati yanakwenda kwenye mfuko wa uzazi (uterus).
Matatizo ya mayai ya uzazi (ovaries) kushindwa kutoa mayai (eggs).
Tatizo la ugumba kwa wanawake husababishwa na;
Matatizo ya autoimmune disorders kama antiphospholipid syndrome (APS)
Matatizo katika uterus na shingo ya kizazi (cervix) kama uvimbe (fibroids or myomas) na birth defects
Matatizo katika mfumo wa kuganda wa damu (clotting disorders).
Mazoezi kupita kiasi (excessive exercise), afya iliyodhoofika (poor nutrition), matatizo ya kula (eating disoder).
Baadhi ya madawa au sumu.
Msongo wa mawazo (emotional stress)
Tatizo la kukosekana kwa usawa wa mfumo wa vichocheo mwilini (hormonal imbalance)
Uzito uliopitiliza (obesity)
Unywaji pombe kupindukia (heavy alcohol intake)
Magonjwa ya muda mrefu kama kisukari (diabetes)
Magonjwa ya kina mama (Pelvic inflammatory infection, PID)
Ovarian cysts and polycytic ovarian syndrome
Magonjwa ya zinaa (sexually transmitted disease, STD) au endometriosis
Saratani
Uvutaji sigara, madawa ya kulevya kama kokeni, bangi, hashishi nk.
Matatizo ya hedhi - wanawake wanaopata hedhi bila kutoa mayai (anovulatory menstrual cycle)
Kuwepo kwa cervical antigens ambazo huua shahawa za mwanamume na hivyo kusababisha kwa mwanamke kutopata ujauzito.
Tatizo la ugumba - linaweza kutokea kwa mwanamume wakati wa;
Kupungua idadi ya shahawa (decrease number of sperm)
Shahawa kuzuiwa kutolewa (blockage of sperm)
Shahawa ambazo hazifanyi kazi yake vizuri.
Kwa mwanamume, tatizo la ugumba husababishwa na;
Mazingira yaliyo na kemikali zinazoathiri uwezo wa mwanaume kumbebesha mimba mwanamke (environment pollutants)
Kukaa sehemu zenye joto kali sana kwa muda mrefu (exposure to high heat)
Matatizo kwenye mfumo wa viashiria vya asili (genetic abnormalities)
Unywaji pombe kupindukia, matumizi ya madawa ya kulevya kama kokeni, bangi, hashishi nk, hupunguza idadi na kiwango (quality) cha shahawa .
Kuzeeka (older age)
Kutumia dawa za vichocheo vya mwilini (hormonal supplements) ama kukosekana kwa baadhi ya vichocheo mwilini (hormonal deficiency)
Kuasiliwa (impotance)
Magonjwa ya korodani (testicular infections) au kwenye mishipa ya korodani (epididymis)
Historia ya matumizi ya baadhi ya dawa za saratani
Magonjwa ya zinaa (STD), ajali (trauma) au upasuaji
Historia ya mionzi (radiation exposure)
Retrograde ejaculation (matatizo ya kukojoa au kutoa shahawa)
Msongo wa mawazo (emotional stress)
Uvutaji sigara
Matumizi ya baadhi ya dawa kama cimetidine, spironolactone, nitrofurantoin.
Varicocele
Mumps
Viashiria na vipimo vya ugumba (infertility)
Kwa wanaume;
Semen analysis - Kipimo hiki kinahusisha uchukuaji wa shahawa kutoka kwa mwanamume ambaye amekaa siku 2-3 bila kujamiana na kuzipima kujua wingi, kiwango chake, shepu zake, viscosity of semen, motility and swimming speed.
Testicular biopsy - Kipimo cha korodani
Kwa wanawake;
Kipimo cha kiwango cha vichocheo kwenye damu (blood hormone levels)
Cervical mucus detection - Kipimo cha kuangalia kamasi za kwenye shingo ya kizazi ili kupima jinsi zinavyovutika (stretch), na kama ni za majimaji (wet) wakati wa mzunguko wa hedhi, na kama zina utelezi ambao huusishwa na ovulatory phase
Kipimo cha kiwango cha joto mwilini (body basal temperature) - Kuongezeka kwa kiwango cha joto kwa 1 degree kutoka kiwango cha joto cha kawaida cha binadamu (37 C) kinahusishwa na ovulation ambapo mwanamke ana asilimia kubwa ya kushika ujauzito au yai limetolewa na ovaries.
Postcoital testing - Kupima kamasi za shingo ya kizazi (cervical mucus) zilizochukuliwa masaa 2-8 baada ya wapenzi kujamiana ili kuangalia mwiingiliano wa shahawa na kamasi za shingo ya kizazi.
Kipimo cha kichocheo aina ya progesterone kwenye damu (serum progesterone testing)
Kipimo cha ukuta wa uterus (biopsy of uterine lining or endometrium)
Kupima kichocheo aina ya Luteinizing hormone kwenye mkojo ili kuweza kutabiri lini yai litatolewa na ovaries ili kupangilia siku za kujamiana kwa wapenzi.
Hysterosalpingography (HSG) - Kipimo cha X-ray kinachotumia dawa maalum (contrast dye) inayoonyesha njia ya shahawa kutoka kwenye shingo ya kizazi kupitia ndani ya mfuko wa kizazi (uterus) na kwenye mirija ya uzazi (fallopian tubes).
Laparascopy - Direct visualization of pelvic cavity
Progestin challenge
Pelvic exam-hufanywa na daktari.
Tiba ya tatizo la ugumba (infertility)
Tiba ni kama ifuatavyo;
Ushauri nasaha na kuwaelimisha wapenzi wawili - Matatizo mengi ya ugumba hutokea kutokana na uelewa au ufahamu mdogo wa elimu ya uzazi na ya kujamiana kwa wapenzi au wanandoa.Kuna wanaume wengi ambao hufika kilele haraka wakati wa kujamiana na hivyo kutoa shahawa mapema (au kukojoa) kabla ya muda muafaka (premature ejaculation), hii husababisha kutopata ujauzito ambapo lawama zote hupelekwa kwa mwanamke pasipo mwanamume kugundua kuwa tatizo ni lake. Ifahamike kwamba hakuna muda uliotengwa ambao ni muafaka wa kufika kilele au kukojoa kwa mwanamume lakini watafiti wa mambo ya kujamiana wanashauri angalau mwanamume afike au akojoe baada ya dakika 15 na kuendelea. Hivyo ni bora kwa wapenzi kujiandaa kisaikolojia mwanzo na kuchezeana kabla ya kuanza kujamiana ili kurefusha muda kwa mwanamume.
Tatizo jengine ni kutofahamu lini hasa ni muda muafaka wa kujamiana ili kushika mimba kwa urahisi. Kuna wanawake ambao hawajui hata mzunguko wao wa hedhi (yaani hawajui wanaanza na kumaliza hedhi lini na wakati wa hedhi wanatumika kwa muda wa siku ngapi). Ongeza nafasi yako ya kushika ujauzito kwa kujamiana angalau mara 3 kwa wiki kuelekea wakati wa ovulation au kujamiana wakati wa kipindi chote cha ovulation. Ovulation hutokea wiki 2 kabla ya mzunguko wako mwengine wa hedhi, kama una mzunguko wa hedhi wa siku 28 (yaani kila baada ya siku 28 unapata hedhi), ni vizuri kujamiana angalau kwa siku 3 kati ya siku ya 7-18 baada ya kupata hedhi.
Kupunguza kunywa pombe kupindukia, kuvuta sigara, kuacha matumizi ya bangi, kokeni nk.
Kupunguza kiwango cha mazoezi kwa wanawake.
Kupunguza unene uliopitiliza
Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu kwani kuwa na wapenzi wengi huongeza athari ya kupata magonjwa ya zinaa.
Kuacha tabia ya kuvaa nguo nzito au zenye kuleta joto kali sehemu za siri kwa wanaume kwani joto kali sana hupunguza kiwango na kuathiri utolewaji wa shahawa.
Kula mlo kamili na wenye virutubisho vyote muhimu kwa afya njema.
Dawa za kutibu magonjwa kwenye mfumo wa uzazi, magonjwa ya zinaa nk.

                  

VIDONDA VYA TUMBO




KATIKA MAKALA HII TUTAANGALI MAMBO MUHIMU MACHACHE JUU YA VIDONDA VYA TUMBO(ULCERS)



“Watanzania wenzangu tumeathirika vya kutosha sasa tuzirudie kanuni muhimu za afya, kama vile hewa safi, maji safi, kiasi, pumziko, lishe bora, mwanga wa jua, mazoezi na kumtegemea Mungu.”

Imeandaliwa na Dr. Cyprian Charles Sizya
                     Tel no; 0627122027
                       Email;cypriansizya@yahoo.com
                             TANZANIA

VIDONDA VYA TUMBO
            Ugonjwa wa vidonda vya tumbo ni ugonjwa ambao unatokana na kumomonyoka (erosion) au kutoboka kwa tabaka la juu la utumbo.Kwa kawaida tabaka la juu la utumbo hulindwa na ukingo maalum (gastric mucosal barrier) kwa kutengeneza ute (mucous) na alkali za madini ya baikaboneti (bicarbonate ions) dhidi ya tindikali na kimeng’enya (enzyme) cha pepsini.
         Mgawanyiko na utengenezwaji wa seli mpya za tabaka la juu la utumbo pamoja na uwepo wa damu ya kutosha ni baadhi ya vigezo vingine vinavyosaidia kulinda tabaka hili na utumbo dhidi ya kumomonyoka au kutoboka
       Kuwepo kwa kigezo chochote kitakachoingiliana na ulinzi dhidi ya tabaka la juu la utumbo hupelekea kumomonyoka kwa tabaka hilo na kusababisha kidonda au vidonda vya tumbo ambavyo huweza kupelekea hata kutoboka kwa utumbo iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa                                                                                                     Kuna dhana iliyozoeleka kuwa vidonda vya tumbo huathiri zaidi mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo (stomach). Dhana hii si kweli kwani sehemu inayoadhiriwa zaidi na tatizo hili ni sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ijulikanayo kama duodenum
Makundi  ya vidonda vya tumbo
Kuna makundi makuu matatu ya ugonjwa huu-
Vidonda vinavyotokea kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo (Gastric ulcers).
Vidonda vinavyotokea kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (Duodenal Ulcers).
 Vidonda vinavyotokea kwenye koo (Oesophageal ulcers)
                                                                                                                                 
AINA YA VIDONDA VYA TUMBO;
 Kuna aina kuu mbili za vidonda vya tumbo;
       1. gastric ulcers, Hii ni Aina ya kwanza ni ile inayoathiri tumbo
        2. peptic ulcers, Aina ya pili ni ile inayoathiri utumbo mwembamba wa duodenam(duodenum).
        Hapo zamani ilikuwepo dhana kwamba msongo wa mawazo (stress) na mlo (diet) husababisha vidonda vya tumbo.Baadaye watafiti wa masuala ya afya ya binadamu waligundua kuwa tindikali izalishwayo tumboni na vimeng’enya vya pepsini inachangia kiwango kikubwa katika kusababisha vidonda vya tumbo.
   Lakinki hivi karibuni utafiti umeonyesha kwamba zaidi ya asilimia themanini ya vidonda vya tumbo hutokana na bakteria aitwaye Heliocobacter pylori (H.pylori). Ingawa inasadikika kwamba vigezo vyote hapo juu huchangia kupata vidonda vya tumbo,bakteria H.pylori anasadikiwa kuwa chanzo kikuu katika kusababisha vidonda vya tumbo.
          
 a)VIDONDA VYA TUMBO (GASTRIC ULCERS) NA DALILI ZAKE
        Asilimia kubwa ya waathirika wa aina hii ya vidonda vya tumbo ni watu wenye umri zaidi ya miaka arobaini (40) na wanaume huathirika zaidi kuliko wanawake.Waathirika wa aina hii ya vidonda vya tumbo huwa wembamba kutokana na kutokula wakihofia kupata maumivu pindi walapo chochote.  Dalili kubwa ya wagonjwa hawa ni;-
maumivu ya tumbo (chembe).Maumivu yake huwa yenye majira maalum ambapo huanza punde tu mgonjwa alapo chakula na hupungua baada ya chakula kuisha tumboni au kwa kunywa kimiminika chenye alkali.
Hamu ya kula huwa nzuri lakini baadhi yao waweza kutapika.Kutapika damu (haematemesis) na kupata choo chenye damu (malaena) huweza kuambatana na aina hii ya vidonda vya tumbo.
Uzito wa mwili hupungua kwa kiasi fulani kutokana na kutokula vizuri.
Kusambaa kwa maumivu mpaka mgongoni kwaweza kutokea iwapo kidonda kimetoboka na kuhusisha kongosho (pancreas).
b)VIDONDA VYA UTUMBO MDOGO (DUODENAL  ULCERS) NA DALILI ZAKE
        Aina hii ya pili kwa upande mwingine huathiri watu wenye umri chini ya miaka arobaini (40) na kama aina ya kwanza,waathirika wengi ni wanaume.
Maumivu yana tofauti na aina ya kwanza, hutokea kati ya masaa mawili na nusu hadi manne bada yamlo ambapo chakula huwa kimeisha tumboni (hunger pains)
.Maumivu pia hutokea zaidi mapema asubuhi au nyakati za jioni.Nafuu hupatikana kwa kula chakula.
Kutapika hutokea kwa nadra sana kwa wagonjwa wa aina hii.
kutapika damu na kupata choo chenye damu hutokea mara nyingi zaidi kuliko aina ya kwanza.
Hamu ya kula kwa wagonjwa wa aina hii huwa nzuri na hupenda kula mara kwa mara hivyo huwa na miili yenye afya nzuri tofauti na wagonjwa wa aina ya kwanza.

        VISABABISHI VYA VIDONDA VYA TUMBO
Vidonda vya tumbo husababishwa na
Maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylori: Imeonekana kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watu duniani wana vimelea hivi katika utumbo. Aidha, miongoni mwao, karibu asilimia 80 huwa hawaoneshi dalili yeyote ya kuugua ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Aina hii ya vimelea vya bacteria husababisha karibu asilimia 60 ya vidonda vinavyotokea kwenye tumbo (gastric ulcers) na zaidi ya asilimia 90 ya duodenal ulcers.
Jinsi H.pylori anavyosababisha vidonda vya tumbo
     Kuathirika na vimelea vya H.pylori ni kawaida kwa mwanadamu yeyote.Takwimu za Uingereza zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia hamsini ya idadi ya watu wazima wameathirika na bakteria hao.Idadi ni kubwa, zaidi ya asilimia tisini, kwa baadhi ya nchi nyingine.
     Hata hivyo ni baadhi tu ya watu kati ya walioathirika na vimelea vya bakteria hawa hupata vidonda vya tumbo.Hakuna sababu za kisayansi zinazoelezea hali hiyo                                                                                                           
            Vimelea vya H.pylori huweza kusambaa kupitia chakula na maji.Vimelea vya bakteria hawa pia hupatikana kwenye mate hivyo vyaweza kuambukizwa kupitia kinywa haswa iwapo mtu atabusiana na muathirika wa vimelea hivyo.Watu wengi pia huathirika na vimelea hivi utotoni.
         Vimelea vya H.pylori huweza kuishi kwenye ute ulindao tabaka la juu la tumbo na utumbo mpana.Hapo hutengeneza kimeng’enya kiitwacho urease ambacho  ambayo hupunguza makali ya tindikali izalishwayo na tumbo yaani gastric juice/acid.Ili kukabiliana na hali hii,tumbo hutengeneza tindikali nyingi zaidi ambayo huathiri tabaka la juu la utumbo.Vimelea hivi pia hudhoofisha ute ulindao tabaka la juu la utumbo hivyo kushindwa kulinda tumbo na utumbo mwembamba sawasawa.
Aidha,vimelea vya H.pylori hujiegesha kwenye seli za tumbo.Hali hii hudhoofisha mfumo wa ulinzi wa tumbo na kusababisha maumivu na hatimaye madhara katika eneo lililoathirika.                                                                                                                                                                                       
      Kushindwa kwa mfumo wa kinga mwilini kuwaua na kuwaondoa kabisa vimelea hawa ndani ya mwili husababisha kuwepo kwa uambukizi wa kudumu katika kuta za tumbo (chronic active gastritis), uambukizi ambao huharibu mfumo na uwezo wa kuta za tumbo kutunza homoni ya Gastrin, ambayo ni muhimu katika kuhakikisha mazingira ya tumbo yanakuwa na kiwango salama cha tindikali.
       Kwa kawaida, kazi ya gastrin ni kuchochea utolewaji wa tindikali (gastric acid) kutoka kwenye seli za ukuta wa tumbo zijulikanazo kama Parietal cells. Iwapo bacteria hawa watashambulia na kuharibu ukuta wa tumbo, mfumo wa gastrin pia huharibika, na hivyo kusababisha gastrin kuzalishwa kwa wingi hali ambayo pia huchochea uzalishaji wa gastric acid kwa wingi. Matokeo ya kuzalishwa kwa wingi kwa tindikali hii hupelekea kuchubuka kwa ukuta wa tumbo na hivyo kusababisha vidonda vya tumbo.
   ii)Matumizi ya dawa muda mrefu .
      Ukuta wa utumbo hujilinda na madhara yatokanayo na tindikali ya utumbo (gastric acid) kwa kuwa na utando laini (mucus) ambao hutolewa na vichocheo vijulikavyo kama Prostaglandins. Dawa mfano za kundi la NSAIDs huharibu mfumo wa kutengeza vichocheo hivi yaani prostaglandins na hivyo kufanya kuta za tumbo kukosa utando wa kuzilinda na mashambulizi ya tindikali hali ambayo hupelekea kutokea kwa vidonda vya tumbo.
iii)Uvutaji wa sigara:
    Uvutaji sigara huchangia kutokea kwa vidonda vya tumbo kwa kiasi fulan,maana sumu ya nikotini na cafein iliyomo ndani ya sigara huamsha uzalishwaji wa tindikali ya gastric kwa wingi na kusababisha kiwango cha tindikali kuwepo kwa wingi  tumboni hali ambayo husababisha ukuta wa utumbo kubabuka/kuchubuka

Iv)Vyakula au viungo vya chakula vyenye uchachu:
       Kinyume na dhana iliyozoeleka miongoni mwa watu wengi, baadhi ya vyakula vyenye uchachu na upilipili kama vile pilipili, ndimu, limao na masala havina uhusiano na uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo..                                                                                                                                         
v)Unywaji wa pombe:
    Unywaji wa pombe pekee hausababishi vidonda vya tumbo. Hata hivyo, unywaji wa pombe sambamba na maambukizi ya vimelea vya Helicobacter pylori huongeza madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo.
vi)Vitu vingine:
      Vitu vinavyohusishwa na uongezaji wa madhara ya vidonda vya tumbo ni pamoja na upasuaji wa tumbo (major abdominal surgeries), kuungua kwa moto (burns), ugonjwa wa figo; na kubadilishwa kwa viungo vya mwili kama figo au ini.
 vii) Msongo wa Mawazo
         Msongo wa mawazo hausababishi vidonda vya tumbo badala yake huongeza maumivu kwenye kidonda kilichopo.Hufanya hivyo kwa kuongeza zaidi utengenezwaji wa tindikali tumboni
Viii) Kafeini (Caffeine)
     Kafeini ambayo hupatikana kwenye baadhi ya vinywaji kama soda, kahawa n.k huchangamsha utengenezaji wa tindikali tumboni ambayo huchubua ukuta wa utumbo na pia hutonesha kidonda kilichopo kama mtu ni mwathirika tayari.
VIASHIRIA VYA VIDONDA VYA TUMBO
 i)Maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe moyo (epigastic pains): Maumivu juu kidogo ya tumbo mara nyingi huendana na muda wa kula chakula. Mtu mwenye vidonda kwenye tumbo (gastric ulcers) hupata maumivu makali sana kipindi anapokula au mara tu baada ya kumaliza kula wakati aliye na vidonda kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenal ulcers) hupata maumivu makali anapokuwa na njaa na hupata nafuu pindi anapokula.
ii)Kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi. Hali hii pia yaweza kuendana na kubeua au kujamba mara kwa mara.
iii)Kucheua na kuongezeka kwa mate yanayoshuka tumboni baada ya kucheua.
iv)Kichefuchefu na kutapika
v)Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito
vi)Kutapika damu,hii hutokea mara nyingi kwa watu wenye vidonda vilivyoko kwnye mfuko wa chakula(gastric ulcers)
vii)Kupata haja kubwa ya rangi nyeusi au kahawia yenye harufu mbaya sana. Hii humaanisha mgonjwa anapata haja kubwa au choo kilichochanganyika na damu kwa mbali
NB:-
Uwepo wa dalili kama kiungulia cha muda mrefu, kucheua na kutapika baada ya kula na historia ya kutumia dawa  kwa muda muda mrefu bila kufuata ushauri wa daktari ni ishara tosha ya kumfanya mgonjwa kumuona daktari kumpima na kumfanyia uchunguzi ili kujiridhisha kuwa hana tatizo la vidonda vya tumbo.
        Ni vyema kumuona daktari ili ufanyiwe uchunguzi na kupatiwa tiba sahihi iwapo una dalili zilizotajwa hapo juu. Pia ni muhimu kuzingatia dozi kwa kunywa dawa katika muda uliopangwa na kumaliza dozi hata baada ya dalili (maumivu) kupotea.
    Ugonjwa wa vidonda vya tumbo tofauti na inavyodhaniwa waweza kupona kabisa kama magonjwa mengine.
Madhara kama kutoboka kwa utumbo,kuvuja damu, kuziba kwa tumbo na saratani ya tumbo yanaweza kutokea iwapo tiba haitatolewa katika muda muafaka.

MADHARA YA VIDONDA VYA TUMBO
   Mgonjwa wa vidonda vya tumbo anaweza kukumbwa na madhara yafuatayo;-
Constipation, yaani kufunga choo au kwenda choo kigumu kama cha mbuzi.
Kukonda/Kudhoofika, hii husababishwa na tumbo kushindwa kusaga chakula kwa kuwa kuna vidonda.
Saratani ya utumbo, pia hii hujitokeza endapo vidonda vitakomaa na kuoza.
Bawasiri/ au mang’ondi, hii husababishwa na viuvimbe vinavyoletwa na mdudu HB.
Tumbo kuuma mara kwa mara kama typhoid, amiba na minyoo
USHAURI KWA MWENYE VIDONDA VYA TUMBO
1. Kula chakula kila baada ya masaa matano hadi sita, kumbuka usile kitu chochote katikati ya muda huo, mfano kama asubuhi umekula saa mbili, unaongeza mbele masaa matano au sita.
2.kunywa maji nusu saa kabla na baada ya mlo, kumbuka maji vuguvugu yafaa zaidi.
3.Epuka kutumia vitu vya baridi, vilivyolala na vya kwenye friji
4.Usitumie vitu vikali kama vile pilipili, limao, tangwizi, n.k
5.Kuwa na ratiba ya chakula isiyobadilikabadilika, ni muhimu kuwa na ratiba ya chakula isiyobadilika(fixed timetable).
6.kunywa maji glasi mbili mara baada ya kuamka na kila baada ya masaa mawili au mara usikiapo njaa.
7.Usitumie vyakula vyenye viungo vingi kama vile pilau, kwani huumiza tumbo.
8.Usiweke vyakula vya aina nyingi kwenye mlo mmoja, na matunda yasitumike pamoja na mboga za majani.
9.fanyamazoezi ya mara kwa mara asubuhi najioni, ususani mazoezi ya asubuhi kulifanya tumbo lako kufanya kazi vyema.
10.epuka kula chakula usiku sana au mida karibu na kulala.
HUDUMA YA KWANZA
Tumia juisi ya papai lililosagwa vizuri kila uonapo maumivu au ifanye kama desturi yako ili kuepusha maumivu makali ya tumbo.
Tumia maji ya vuguvugu pamoja na asali glasi moja kila baada ya masaa manne, na ifanye kama desturi yako.
Kama tumbo limekusababishia kuhara na kutoa damu chukua mkaa saga weka kwenye kikombe, tia na limao kidogo kunywa na m aji moto
LISHE KWA AJILI YA VIDONDA VYA TUMBO
CHARDANS FOOD
Hii ni lishe nzuri sana kwa wale ambao matumbo yao yanashindwa kumeng’enya chakula vizuri na kujikuta wanapata kilungulila baada ya kula.
     Mahitaji
Kilo moja ya viazi mbatata
Mimea miwili ya vitunguu
  Maandalizi
Osha viazi vyako usivimenye
Vikate viazi vyako katikati
Katakata majani ya vitunguu vyako na uweke kwenye dishi
Tia viazi na chumvi ndani ya dishi pamoja na vitunguu
Chemsha kwa pamoja kwa joto la nyuzi 220
Kisha toa tayari kwa matumizi.
Nb;- hii lishe inasidia tumbo, na kusaidia moyo usipate high blood pressure, na kusaidia kutoa sumu kwenye figo.
FRUIT SALAD
Hii ni lishe safi sana inalisaidia tumbo kuua vijidudu, vya minyoo, amiba, homa ya matumbo, UTI, pia husaidi kutoa mafuta mwilini
       Mahitaji
Limao
Vitunguu swaumu na maji
Karoti
Tango
       Maandalizi
Vioshe vyote kwa maji moto
Menya limao kisha katakata vipande, usitoe mbegu
Katakata vitunguu vipande vidogo vidogo
Katakata karoti na tango vipande vidogodogo bila kuvimenya
Changanya vyote kwenye sahani
         Matumizi
Tumia walau vijiko nane kutwa mara mbili kila baada ya masaa nane
Mara umalizapo kutumia usinywe maji wala kula chochote mpaka baada ya dakika 45.
TIBA YA ULCERS
       Matibabu ya tatizo hili uchukua takribani wiki sita hadi wiki ishirini na nne, hivyo mgonjwa wa namna hii ni vema akifika kituoni, apimwe ili kusudi tujue kuwa, vidonda ni vya aina gani na vipo katika hatua ipi.
   Wengi wanadhana potofu kichwani mwao kuwa mtu hawezi kupona vidonda vya tumbo, mimi nakubaliana nao, kuwa ni kweli huwezi kupona kwa kuwa hauwezi kuzingatia kanuni za afya, lakini kwa wale wanaozingatia kanuni za afya kupona ni haraka na rahisi, njoo uwe shuhuda kwa wengine.
JAMB O MUHIMU KWETU
       Kujua jinsi ya kujikinga na tatizo ni vyema sana kuliko kujua namna ya kujitibu, hivyo ni vyema turejee kwenye kanuni ambazo Mungu mwenyewe alituwekea kwa ajili ya uponyaji wa afya zetu kwani anahitaji tuwe wazima kimwili na kiroho, ndugu yangu hebu chukua hatua na uzingatie kanuni za afya ambazo ni;-  hewa safi, maji safi, lishe bora, pumziko, mazoezi, mwanga wa jua, kiasi na kumtegemea MUNGU.

Tuesday, 7 June 2016

ZIJUE FAIDA ZA MLONGE




KAMA kuna mti wenye faida nyingi za kiafya, basi Mlonge unaweza kuwa unaongoza. Kila eneo la mti huu, kuanzia majani, maua, mbegu, magamba hadi mizizi yake ina virutubisho vya kipekee vyenye faida nyingi za kiafya kwa binadamu.
Majani ya Mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga wake unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika moja lijulikanalo kama Trees For Life, majani ya Mlonge yana Vitamin A nyingi kuliko karoti, vitamin C nyingi kuliko machungwa na madini ya Potassium nyingi kuliko ndizi mbivu, halikadhalika ubora wa protini yake ni bora kushinda maziwa na mayai.
Kutokana na kuwa na kiasi kingi cha madini ya chuma  (Iron), kasiamu (Calcium) na vitamin nyingi za aina mbalimbali, majani ya mmea huu yamekuwa yakitumika kama ‘tonic’ kwa watoto wadogo na vijana ili kuimarisha mifupa na kusafisha mfumo wa damu mwilini.
Ili kutengeneza ‘tonic’, saga majani mabichi ya Mlonge pamoja na maji, yachuje kisha changanya na maziwa halisi. Inaelezwa kuwa juisi ya aina hii ni dawa nzuri kwa waja wazito, kwani huboresha njia ya uzazi na kumuwezesha mama kuzaa bila matatizo na kuondoa matatizo baada ya kujifungua.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, mti wa Mlonge unatibu karibu magonjwa 300 ya aina mbalimbali, yakiwemo yale magonjwa sugu, baadhi yake ni kama haya yafuatayo:
Mlonge unaweza kutibu Pumu, Kikohozi na Kifua Kikuu. Aidha, magonjwa mengine kama Kisukari, Shinikizo la damu (la juu na chini), magonjwa ya ngozi, magonjwa ya kwenye njia ya mkojo (UTI) kuongeza kinga ya mwili (CD4) na kuongeza nguvu za kiume.